22 Mei 2017 - 21:52
Trump apandikiza chuki dhidi ya mataifa ya kiislam

Hotuba ya Trump katika mji wa Riyadh nchini Saudi Arabia ilikuwa na lengo la kupandikiza chuki na kuchochea matatizo katika nchi za kiislamu, ambapo amejitahidi kutia chuki kwa mataifa ya kiarabu dhidi ya jamhuri ya kiislam ya Iran.

Shirika la habari la habari la ABNA linaripoti kuwa: Hotuba ya Trump katika mji wa Riyadh nchini Saudi Arabia ilikuwa na lengo la kupandikiza chuki na kuchochea matatizo katika nchi za kiislamu, ambapo amejitahidi kutia chuki kwa mataifa ya kiarabu dhidi ya jamhuri ya kiislam ya Iran.

Baina ya kile kilichotokea Tehran na Riyadh pana tafauti kubwa. Mjini Riyadh, anaonekana Donald Trump akicheza ngoma ya upanga, ngoma ya vita, huku Mfalme Salman akimpa maelekezo rais huyo wa Marekani.

Kwa upande mwingine, mjini Tehran, watu nako wanacheza ngoma hiyo mabarabarani wakishangilia ushindi mkubwa wa Rais Hassan Rouhani anayeelemea siasa za wastani dhidi ya mpinzani wake, Ebrahim Raisi, anayependelea siasa za msimamo mkali.

Furaha imetanda katika ufalme wa Saudi Arabia, ulio na utajiri wa mafuta. Hotuba ya jana ya Trump imezindua mabadiliko mapya katika sera za Marekani kuelekea dunia ya Kiarabu kwa jumla pamoja na lawama za Saudi Arabia dhidi ya rais aliyemaliza muda wake nchini Marekani, Barack Obama. Hotuba hiyo ni kama imefikisha mwisho yote hayo yaliyokuwepo.

Wakati huo huo, mkakati ya kijeshi dhidi ya wapinzani wakuu, Iran, kama ilivyokuwa wakati wa rais wa zamani wa Marekani, George W. Bush kwamba jamhuri  ya kiislamu ya Iran ilichukuliwa ni la watu wabaya waliopaswa kutengwa. 

Na kwa kuwa kutengwa peke yake huenda kukawa ni hatua ambayo haitoshi, Trump ameongezea mikataba ya mauzo ya silaha yenye thamani ya dola bilioni 110 katika yale aliyobeba kwenye ziara yake hiyo ya Saudi Arabia, ambayo kwa kweli ni historia katika biashara. Saudia Arabia inazitumia silaha hizo kuwaangamiza wananchi wa Yemen na kuwasaidia magaidi nchini Syria na Iraq.

Ni kejeli na machungu katika nchi ya Saudia Arabia ambayo ni nyumbani kwa magaidi waliohusika na mauaji ya tarehe 11 mwezi Septemba mwaka 2001, kukuta kuwa Trump anaishutumu Iran ambayo haijahusika na ugaidi kwamba ndiyo inayounga mkono na kusaidia vitendo vya kigaidi.

Lakini haijawahi kutajwa kwamba  Saudia Arabia na nchi za Ghuba wamekuwa wakiwapa msaada wa fedha na silaha wapiganaji wa kundi la kigaidi la Daesh linalojiita Dola la Kiislamu, IS, pamoja na makundi mengine ya jihadi, kwani hata aliyekuwa Makamu wa Rais wa Marekani, Joe Biden, alitamka wazi wazi  juu ya kutoa msaada kwa magaidi, wakati alipozungumza na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Harvard mnamo mwaka 2014.

Kwenye hotuba yake, Trump alizungumzia kuhusu amani, usalama na ustawi katika kanda hiyo. Kama kweli angalikuwa na mtazamo kama huo, mambo yangalikuwa tofauti. Kutokana na uadui wa kimkakati uliopo kati ya Iran na Saudi Arabia, hakuna tamko lolote lililoashiria kujiepusha na makabiliano au hata kuwepo na usawa.

Badala yake, rais huyo wa Marekani anachochea mapambano. Ingawa hotuba ya Trump iligusia Iran, lakini hakugusia hata kidogo juu ya mwelekeo wa uchaguzi wa Iran.

Badala ya kutafuta Amani na suluhu, Trump amezidi kuwatia hofu Wasaudi kwamba Iran ina nguvu na ushawishi katika eneo hilo.

Kimakusudi Trump  ameviunga mkono wazi vita na mauaji ya mataifa ya Ghuba katika nchi ya Yemen kama sehemu ya "vita dhidi ya ugaidi".

Kama kweli Trump angelikuwa makini kuhusu nia yake kuwa watoto, wavulana na wasichana wanastahili kukua bila hofu, wanastahili kulindwa kutokana na vurugu na chuki, basi kamwe asingeweza kuiunga mkono Saudi Arabia. Hotuba ya Trump imebashiri ukweli mmoja tu, nao ni kuwa hana  nia njema na waislamu hawa wa mataifa ya kiarabu. Lazima bara hili likatae kucheza ngoma ya upanga. Licha ya kuendelea kwa miito ya kuiwekea Iran vikwazo zaidi, pana ulazima wa kuanzisha majadiliano na kufungua njia za kiuchumi kwa Tehran.

Ulimwengu lazima ujaribu kufanya mazungumzo ya kikanda ili kuanzisha mbinu mpya za usalama ambazo zitazingatia maslahi ya pande zote husika. Usalama katika eneo la Mashariki ya Kati ni zaidi ya mchezo uliokwenda kapa. Ndio maana ilikuwa ishara nzuri pale mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya, Federica Mogherini, alipompongeza Hassan Rouhani kwa kuchaguliwa tena kuwa rais.

Mwisho wa habari/ 291